Home Habari Kuu NACADA yaagiza kutolewa kwa mabango ya vileo karibu na taasisi za elimu

NACADA yaagiza kutolewa kwa mabango ya vileo karibu na taasisi za elimu

0

Shirika la kupambana na dawa za kulevya na matumizi ya pombe nchini- NACADA, limeagiza maajenti wa matangazo ya kibiashara kutoa mabango yote ya vileo yaliyo karibu na taasisi za elimu.

Akizungumza jijini Nairobi Jumatatu, afisa mkuu wa shirika hilo Anthony Omerikwa, alisema hatua hiyo inalenga kuboresha maisha ya halafu ya vijana kwa kuwaepusha na vileo na bidhaa zingine haramu.

”Kuwepo Kwa matangazo ya pombe karibu na taasisi za elimu, kunadunisha maisha ya baadaye Kwa kufanya kawaida unyuaji wa pombe na pia kuonekana chaguo nzuri”, alisema Omerikwa.