Nasreddine Nabi ameteuliwa kuwa meneja mpya wa mabingwa wa ligi kuu ya Morocco FAR Rabat, baada ya kugura miamba wa Tanzania Young Africans almaarufu Yanga.
Raia huyo wa Tunisias alien a umri wa miaka 57 alizinduliwa Jumanne tayari kwa msimu mpya wa ligi ya mabingwa Afrika.
Nabi aliondoka Yanga mwezi uliopita baada ya kukamilisha kondrati yake ya miaka mitatu ambapo alinyakua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mara mbili mtawalia mwaka 2020 na 2021 ,mataji amwili ya shirikisho na kucheza hadi fainali ya kombe la shirikisho la soka Afrika.
Nabi amesaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo ya kijeshi ambayo ni mojawapo wa klabu zenye ufanisi mkubwa nchini Morocco, wakijivunia kuwa timu ya kwanza kutoka taifa hilo la kaskazini mwa Afrika kunyakua kombe la ligi ya mabingwa Afrika mwaka 1985.