Home Kimataifa Mzozo wa Sudan: Shambulio la anga dhidi ya Khartoum laua takriban watu...

Mzozo wa Sudan: Shambulio la anga dhidi ya Khartoum laua takriban watu 20

0

Shambulizi la anga la jeshi katika mji mkuu wa Sudan limeua takriban watu 20, wakiwemo watoto wawili, wanaharakati wanasema.

Wengi wa wahasiriwa wa shambulio hilo, katika kitongoji cha Kalakla al-Qubba kusini-magharibi mwa Khartoum, wamezikwa kwenye vifusi, walisema.

Milio ya risasi na roketi imeripotiwa katika maeneo kadhaa siku ya Jumapili.

Jeshi na wanajeshi wa Rapid Support Forces (RSF) wamekuwa wakipigania udhibiti wa mji wa Khartoum tangu Aprili. Mamia wameuawa.

Wizara ya afya nchini humo inasema zaidi ya watu 1,100 wamefariki katika maeneo mbalimbali nchini humo lakini idadi halisi huenda ikawa kubwa zaidi.

Raia wengi wamenaswa katika mapigano hayo.

Takriban watu milioni 2.2 wametoroka makazi yao ndani ya Sudan na zaidi ya nusu milioni wametafuta hifadhi katika nchi jirani, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Mzozo huo ulianza baada ya mkuu wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na mkuu wa RSF Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo kutofautiana kuhusu mustakabali wa nchi.

Mikakati kadhaa ya kusitisha mapigano imetangazwa kuruhusu watu kutoroka mapigano lakini hayajazingatiwa.

BBC
+ posts