Home Kaunti Mzozo wa ndizi wasababisha kifo Tharaka Nithi

Mzozo wa ndizi wasababisha kifo Tharaka Nithi

0
kra

Polisi katika kaunti ya Tharaka Nithi wanachunguza tukio la kuuawa kwa mwanamume wa umri wa miaka 36 alipodai malipo ya ndizi ya shilingi 50.

Inadaiwa kuwa, Lloyd Muigai alishuku mmoja wa jamaa wake kuwa aliyechukuwa ndizi kutoka kwa mgomba wake hivyo akamuuliza. Majibizano makali yalizuka na kusababisha Muigai kuwaita wanafamilia waliomfunga kwa kamba na kuanza kumpiga kwa zamu.

kra

Kufuatia hali hiyo, alipiga ukemi mkali wa kutaka msaada. Majirani waliusikia na wakaja ila juhudi za kumwokoa Muigai zilizimwa na waliomvamia.

Alipopata habari hiyo, chifu wa tarafa hiyo aliandamana na polisi hadi eneo la mkasa na kuthibitisha kuwa Muigai alifariki kutokana na majeraha.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Chuka huku sita waliohusika na tukio hilo wakitiwa mbaroni na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Chuka.

Boniface Mutotsi
+ posts