Home Habari Kuu Mzozo wa Jubilee waendelea, mrengo wa Uhuru wakimbia mahakamani...

Mzozo wa Jubilee waendelea, mrengo wa Uhuru wakimbia mahakamani kutafuta haki

0

Mzozo wa chama tawala cha zamani Jubilee unaonekana kuendelea kutokota, baada ya mrengo wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, kuwasilisha kesi katika mahakama ya Milimani siku ya Ijumaa dhidi ya Mbunge Mteule Sabina Chege na Mbunge wa EALA Kanini Kega.

Mrengo wa Rais mstaafu unawashutumu wawili hao kwa kuendelea kuchangia mgawinyo wakijidai kuwa viongozi wa chama Jaji Janet Mulwa, amesema kesi hiyo ni ya dharura na itasikizwa Oktoba 23 mwaka huu.

 

Website | + posts