Home Habari Kuu Mzalendo Kibunjia akanusha kushiriki ufisadi

Mzalendo Kibunjia akanusha kushiriki ufisadi

Wengine waliokamatwa na Kibunjia ni pamoja na Stanvas Ongalo, Oliver Rabuor, Wycliffe Ongaya na Oscar Mwaura.

0

Aliyekuwa Mkurugenzi wa makavazi ya kitaifa humu nchini Mzalendo Kibunjia na watu wengine wanne wamefikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kufuja shilingi Milioni 441,fedha za umma.

Aidha wanne hao walikamusha mashtaka hayo na wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi Milioni tano kila mmoja, au bondi ya shilingi Milioni 10 na mdhamini wa kiwango sawa na hicho.

Wengine waliokamatwa na Kibunjia ni pamoja na Stanvas Ongalo, Oliver Rabuor, Wycliffe Ongaya na Oscar Mwaura.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, pesa hizo za umma zililipwa kwa njia ya udanganyifu kama mishahara na marupurupu kwa watu wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa makavi ya kitaifa humu nchini.

Stanvas ni mkurugenzi wa idara ya masuala ya wafanyakazi na usimamizi, ilhali Oliver ni afisa wa malipo huku Wycliffe akiwa mhasibu wa mishahara.

Wametakiwa kuwasilisha stakabadhi zao za usafiri kwa mahakama na kutowasiliana na mashahidi ambao watatumika na upande wa mashtaka.

Website | + posts