Msanii wa Marekani Fatman Scoop amefariki akiwa na umri wa miaka 53 baada ya kuanguka na kuzirai akiwatumbuiza mashabiki siku ya Ijumaa.
Kulingana na shirika la utangazi nchini Uingereza BBC,Scoop alikuwa katikati ya tamasha lake mjini Hamden nchini Marekani alipozirai na kukimbizwa hospitalini .
Hata hivyo yamkini msanii huyo alifariki punde alipowasilishwa hospitalini na Ambulensi.
Scoop ni msanii mashuhuri nchini Marekani akipiga mziki chapa ya Hip Hop tangu miaka ya 90 na alikuwa ameshinda tuzo kadhaa.