Home Burudani Mwimbaji Pete Odera ashinda tuzo ya Stellar nchini Marekani

Mwimbaji Pete Odera ashinda tuzo ya Stellar nchini Marekani

0
kra

Mwimbaji wa nyimbo za injili Daktari Pete Odera amejiongezea tuzo baada ya kushinda nyingine katika tuzo za Stellar awamu ya 39 zilizoandaliwa huko Las Vegas, Nevada nchini Marekani.

Odera alishukuru wasikilizaji wake wengi kwa kuiweka Kenya kwenye ramani ya ulimwengu ya nyimbo za injili na kwa kuifanyia haki Afrika kwa kuunga mkono muziki wake.

kra

Kituo cha redio kwa jina GODRADIO1 ambacho hupeperusha kipindi chake cha kila wiki kiitwacho “Good Morning Africa” kilishinda vituo vingine vya redio vya Marekani na vya sehemu mbali mbali ulimwenguni na kunyakua tuzo ya kituo cha redio cha mtandaoni cha mwaka.

Daktari Pete Odera na wafanyakazi wenzake Walter KO, Robert Earl Dean na mwelekezi wa kipindi Michelle Thompson walichukua tuzo hiyo wakati wa dhifa ya walioteuliwa kuwania tuzo hizo katika ukumbi wa hoteli ya Palm Resort Julai 19, 2024.

Tye Tribbett alinyakua tuzo ya wimbo wa mwaka huku mwekelezi wa kwaya ya nyimbo za injili Ricky Dillard akibeba ile ya kwaya ya mwaka.

Jaji Kim Burrell ambaye hujuhusisha na mazoezi ya mwili na ambaye pia ni jaji wa BET alitunukiwa tuzo ya Aretha Franklin ya nyota wa mwaka.

Website | + posts