Home Burudani Mwimbaji Marco Joseph wa kundi la Zabron Singers afariki

Mwimbaji Marco Joseph wa kundi la Zabron Singers afariki

0
Mwimbaji Marco Joseph aliyefariki kutokana na matatizo ya moyo
kra

Mwimbaji Marco Joseph wa kundi maarufu la nyimbo za injili la Zabron Singers kutoka Tanzania ameaga dunia.

Marco alifariki juzi Jumatano wakati akipokea matibabu katika Taasisi ya Matibabu ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika hospitali ya kitaifa ya Muhimbili.

kra

Mwimbaji huyo aliripotiwa kuugua uugonjwa wa moyo wiki moja iliyopita.

Hali hiyo ilimlazimu kutoambatana na wenzake waliokuwa wakifanya ziara humu nchini ili kueneza injili kupitia nyimbo zao.

Hii ni baada ya kubainika kuwa alikuwa na tatizo la moyo na alihitaji kufanyiwa upasuaji.

Wandani wake waliozungumza na waandishi wa habari baada ya kifo chake walisema Marco alianza kupata ugumu wa kupumua takriban wiki moja iliyopita.

Baadhi ya nyimbo maarufu zilizoimbwa na kundi la Zabron Singers na kulifanya kujizolea umaarufu ndani na nje ya Tanzania ni pamoja na Sweetie Sweetie ambao umeibuka kutikisa anga wakati wa sherehe za harusi, Mkono wake Bwana na Sisi Ndio Wale.

Mwenyezi Mungu na ailaze roho ya Marco Joseph mahali pema peponi.

Website | + posts