Home Burudani Mwimbaji Emmy Kosgey asherehekea miaka 10 ya ndoa

Mwimbaji Emmy Kosgey asherehekea miaka 10 ya ndoa

0

Mwimbaji wa asili ya Kenya Emmy Kosgey anasherehekea miaka kumi ya ndoa yake na mhubiri maarufu wa Nigeria Anselm Madubuko. Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2013.

Kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, Kosgey alimsifia mume wake akimtaja kuwa aliye na moyo wa dhahabu na ambaye ameongeza thamani kubwa kwa maisha yake.

Waliandaliwa sherehe na washiriki wa kanisa lao kulingana na video aliyochapisha mwimbaji huyo ambapo wanaonekana wakiimba na kucheza kwa furaha.

Aliandika, “Ninaloweza kusema ni Asanye Yahweh. Miaka kumi sasa na tunaendelea vyema. Ninafurahia kwamba nilikubali kuolewa nawe. Tangu nilipoanza safari ya imani katika Mungu kumfuata Boaz wangu hadi nchi ya mbali nisijue alichonipangia Mungu, imekuwa safari ya ufichuzi wa mawazo ya Mungu na maisha yenye kusudi.”

Alipohojiwa yapata miaka 7 iliyopita Emmy alielezea jinsi walikutana na mtumishi huyo wa Mungu. Alisema walikutana kwenye kongamano la injili nchini Kenya wakawa marafiki na akamwalika kwa kongamano jingine huko Uingereza.

Wakati huo ndio mke wa Madubuko aliaga dunia na uhusiano wao ukaanza.

Website | + posts