Home Habari Kuu Mwili wa Tom Osinde wapatikana Migori

Mwili wa Tom Osinde wapatikana Migori

0

Mwili wa afisa wa zamani wa Wizara ya Fedha Tom Osinde umepatikana kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya kaunti ya Migori.

Mwili wa Osinde aliyetoweka wiki mbili zilizopita umekuwa kwenye chumba hicho tangu Alhamisi wiki iliyopita.

Maafisa kutoka kituo cha polisi cha Kamagambo waliutoa mwili huo katika mto Kuja katika kaunti ya Migori wiki jana lakini maafisa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya kaunti ya Migori hawakufahamu ulikuwa wa Osinde.

Polisi wanasema wamekusanya ushahidi muhimu utakaowasaidia katika uchunguzi.

Osinde alitoweka Juni 18 wakati akisafiri kutoka nyumbani kwake mjini Nakuru kuelekea Borabu katika kaunti ya Kisii.

Wafanyakazi wawili ambao wamekuwa wakimhudumia Osinde katika shamba lake lililopo eneo la Ngata mjini Nakuru kwa sasa wanazuiliwa na polisi huku mmoja wao akisemekana kuwa mshukiwa mkuu.

Akizungumza na KBC kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi wa kaunti ya Migori Peter Kimani alisema mwili huo ulikuwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Migori kama ule wa mtu asiyetambuliwa hadi kijana yake alipoutambua kuwa wa baba yake mapema siku ya Alhamisi.

Kimani amesema uchunguzi unaendelea kwa sasa ukifanywa na wapelelezi kutoka kaunti za Nakuru na Migori.

Tom Osinde ni kaka yake marehemi Ken Osinde ambaye alikuwa Mkuu wa zamani wa Wafanyakazi katika afisi ya Rais William Ruto wakati huo akihudumu kama Naibu wa Rais.

Taarifa ya John Kioria na Kennedy Epalat

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here