Home Kimataifa Mwili wa Ogolla wawasilishwa nyumbani kwake tayari lwa mazishi

Mwili wa Ogolla wawasilishwa nyumbani kwake tayari lwa mazishi

0
kra

Mwili wa marehemu Mkuu wa majeshi Jenerali Francis Ogolla umewasilishwa nyumbani kwake kauntinya Siaya tayari kwa mazishi.

Ogolla alifariki siku ya Alhamisi kupitia ajali ya ndege na maafisa wengine tisa wa jeshi katika kaunti ya ElgeyoMarakwet.

kra

Mazishi hayo ya Jumapili yanahudhuriwa na Rais William Ruto na viongozi wengine wa kidiplomasia.

Rais Ruto amewasili Siaya kuhudhuria mazishi hayo.

Ibada ta wafu kwa marehemu Ogolla iliandaliwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex na kuongozwa na Rais Ruto.

Marehemu Ogolla amemwacha mjane na watoto wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume.

Website | + posts