Home Habari Kuu Mwili wa Navalny wakabidhiwa mamake mzazi

Mwili wa Navalny wakabidhiwa mamake mzazi

0
kra

Mwili wa mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny umerejeshwa kwa mama yake mzazi. Haya ni kulingana na msemaji wa Navalny.

Hatua hii inafuatia taarifa za awali kwamba mama huyo alikuwa ameshurutishwa kukubali kumwandalia mwanawe mazishi ya siri la sivyo azikwe katika gereza alilokufia.

kra

Msemaji wa Navalny kwa jina Kira Yarmysh alitumia akaunti yake ya mtandao wa X kushukuru wote ambao walisimama nao katika kuitisha mwili huo.

Yarmysh alisema pia kwamba bado mazishi hayajaandaliwa na hawajui iwapo serikali itaingilia na kuvuruga mazishi kwa jinsi yatakavyopangwa na familia ya Navalny.

Mapena jana Jumamosi, mkewe Navalny kwa jina Yulia, alilaumu serikali ya Rais Vladimir Putin kwa kuzuilia mwili wa mume wake akataka uachiliwe bila masharti yoyote.

Yulia alishtumu Rais wa Urusi kwa kuhusika na mauaji ya mume wake, madai ambayo yamekanushwa vikali na afisi ya Rais.

Afisi hiyo ya Rais imetaja malalamiko ya nchi za magharibi kuhusu kifo cha Navalny kuwa kama mpagao.

Alexei Navalny alikufa Februari 16, 2024, katika jela ya Urusi ya Arctic Circle.

Website | + posts