Mamlaka za Marekani na Kenya zinamsaka muuaji wa mwanamke Mkenya mwenye aliye pia na urai wa Marekani aliyepatikana amefariki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Boston Logan huko Massachusetts.
Polisi walisema waliupata mwili uliokuwa na majeraha wa Margaret Mbitu, 31, kwenye kiti cha abiria cha gari lililokuwa limeegeshwa kwenye uwanja wa ndege.
Mshukiwa mkuu ni mpenzi wa Mbitu, Kevin Kangethe, ambaye inaaminika alikimbilia Kenya baada ya kuuacha mwili wake kwenye uwanja wa ndege.
Mamake Mbitu aliambia kituo cha Boston 25 News kwamba binti yake amekuwa akijaribu kukatisha uhusiano wake na Kangethe.
Mbitu alionekana akiwa hai mara ya mwisho alipoondoka kazini Jumatatu usiku.