Home Burudani Mwigizaji wa Nigeria Mr. Ibu kuzikwa Juni 28

Mwigizaji wa Nigeria Mr. Ibu kuzikwa Juni 28

0

Mwigizaji maarufu wa sinema ya Nigeria John Okafor almaarufu Mr. Ibu atazikwa Juni 28 mwaka huu takriban miezi mitatu tangu kifo chake.

Tarehe ya mazishi imetengazwa na nduguye marehemu Sunday Okafor,akiongeza kuwa wanapanga kuandaa mazishi ya taathima ndio maana wakachelezesha kumzika..

Kulingana na ratiba hiyo mipango ya mazishi itaanza Juni 25 kwa mchuano wa soka wa kumkumbuka marehemu ukifuatwa na sherehe ya kuwasha mishumaa na burudani kutoka kwa bendi mbalimbali Juni 26 maarufu kama Mr Ibu’s Night.

Juni 27 kutaandaliwa na kesha nyumbani kwa marehemu eneo la Nkanu West .

Mr Ibu ameigiza kwenye sinema zaidi ya 200 za Nigeria .

Website | + posts