Home Burudani Mwigizaji wa Korea Kusini Lee Sun-kyun afariki

Mwigizaji wa Korea Kusini Lee Sun-kyun afariki

0
kra

Mwigizaji wa Korea Kusini Lee Sun-kyun ambaye wengi wanamfahamu kwa kuhusika kwenye filamu iliyoshinda tuzo ya Oscar “Parasite” amepatikana akiwa amefariki.

Polisi walielezea kwamba Lee wa umri wa miaka 48, alipatikana ndani ya gari katika hali ambayo mwanzo walidhania kwamba ni kupoteza fahamu na baadaye wakagundua alikuwa amekata roho.

kra

Gari hilo lilikuwa katika mojawapo ya maegesho makuu ya magari mjini Seoul.

Maafisa hao wa usalama hawakubainisha iwapo alijitoa uhai lakini walikuwa wamepokea ripoti kwamba alikuwa ameondoka nyumbani na kuacha ujumbe ambao ulionekana kama wa kujitoa uhai.

Lee amekuwa akichunguzwa kwa kosa la matumizi ya dawa za kulevya zilizoharamishwa nyumbani kwa mhudumu mmoja wa baa tangu Oktoba, 2023.

Alijitetea akisema alihadaiwa kutumia dawa hizo na akashtaki watu wawili akiwemo mhudumu huyo wa baa kwa usaliti.

Polisi sasa wamesema wanasitisha uchunguzi kuhusu matumizi ya dawa hizo za kulevya dhidi ya Lee lakini wataendelea kuchunguza watu wawili ambao aliwashtaki.

Katika filamu ya Parasite, Lee aliigiza kama baba wa familia tajiri ya Park ambayo iliingiliwa na watu wa familia fulani maskini.

Ilishinda tuzo nne za Oscars.

Lee ameacha mke wake Jeon Hye-jin ambaye pia ni mwigizaji na watoto wawili wa kiume.

Website | + posts