Home Burudani Mwigizaji wa Kenya Justin Mirichii ateuliwa kuwania tuzo ya AMAA

Mwigizaji wa Kenya Justin Mirichii ateuliwa kuwania tuzo ya AMAA

0

Mwigizaji wa Kenya Justin Mirichii ameteuliwa kuwania tuzo ya Africa Movie Academy (AMAA).

Msanii huyo amekuwa akiigiza katika filamu tangu mwaka 2008  zikiwemo Disconnect 2, iliyofanya vyema na kumaliza katika kumi bora katika mtandao wa Netflix katika orodha ya nchi 16.

Filamu zake nyingine ni Shimoni aliyoitoa mwaka jana ambapo ndiye mwigizaji mkuu.

Mnamo mwaka 2016, alinyakua tuzo ya mwigizaji bora katika filamu ya ‘48-Hour Film Project’ katika tuzo za Kalasha.

Tuzo hiyo itaandaliwa mjini Lagos nchini Nigeria Oktoba 29 mwaka huu.