Home Burudani Mwigizaji Charles Ouda afariki

Mwigizaji Charles Ouda afariki

0

Mwigizaji wa muda mrefu nchini Kenya Charles J. Ouda amefariki akiwa na umri wa miaka 38. Familia yake na mpenzi wake Ciru Muriuki walitangaza kifo chake.

Kulingana na taarifa hiyo, Charles aliaga usiku wa Jumamosi, Februari 3, 2024 ila haikutoa habari kuhusu kilichosababisha kifo hicho.

Haya yanajiri miezi sita pekee tangu Charles na Ciru walipotangaza kwamba wako kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Familia ya Ouda na Ciru wameomba wapatiwe muda wa kuomboleza mpendwa wao lakini wameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.

Wengi wanamfahamu Charles Ouda kutokana na jukumu lake katika kipindi cha Makutano Junction ambacho kilionyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye runinga ya KBC.

Website | + posts