Home Burudani Mwigizaji Amaechi Muonagor amefariki

Mwigizaji Amaechi Muonagor amefariki

0

Mwigizaji wa filamu za Nigeria Amaechi Muonagor amefariki. Kifo chake kinaripotiwa kutokea Jumapili Machi 24, 2024.

Amekuwa akiugua ugonjwa wa figo, kisukari na kiharusi pia.

Mwaka jana aliugua kiharusi ambacho kilisababisha sehemu ya mguu wake wa kushoto kupooza.

Ameaga siku chache tu baada ya video yake akiomba msaada wa kifedha kugharamia matibabu, kusambaa mitandaoni.

Mpango aliokuwa nao ni wa kubadilishiwa figo lakini sasa ameaga dunia.

Yeye ni mmoja wa wazee tajika katika fani ya uigizaji nchini Nigeria ambapo amekuwa akipatiwa majukumu ya kuigiza kama baba kwenye filamu nyingi tu.

Haya yanajiri siku chache baada ya kifo Cha mwigizaji mwenzake John Okafor almaarufu Mr. Ibu.

Website | + posts