Mwenyekiti wa zamani wa Mamlaka ya Ustawishaji wa Chai Nchini, KTDA David Muni Ichoho ameondoa kesi aliyokuwa amewasilisha mahakamani kupinga madai ya kuondolewa kwenye wadhifa huo.
Ilani ya uondoaji wa kesi hiyo iliwasilishwa na mawakili wake katika Kitengo cha Mapitio ya Sheria katika Mahakama Kuu.
“Zingatia kwamba aliyewasilisha mashtaka anawasilisha ilani ya kuyaondoa dhidi ya washtakiwa,” Ichoho aliiambia mahakama.
Ichoho alikuwa amewaorodhesha wanachama wa Bodi ya KTDA, katibu wa kampunii hiyo na Afisa Mkuu Mtendaji kama washtakiwa akidai walimshinikiza kujiuzulu kama mwenyekiti wa bodi ili kutoa fursa ya kufanywa kwa mabadiliko ya uongozi kwenye kampuni hiyo.
Kuondolewa kwa kesi hiyo kunakuja wiki moja baada ya KTDA kutangaza kuteuliwa kwa Enos Njiru Njeru kuwa mwenyekiti wake wa kitaifa kuanzia Julai 17, 2023 kufuatia kujiuzulu kwa David Ichoho.