Home Habari Kuu Mwanzilishi wa taasisi ya NIBS aaga dunia

Mwanzilishi wa taasisi ya NIBS aaga dunia

0

Lizzie Wanyoike ambaye anafahamika sana nchini Kenya kwa kuanzisha taasisi ya “Nairobi Institute of Business Studies” almaarufu NIBS ameaga dunia.

Familia yake ilithibitisha kifo chake jana Jumapili, Januari14, 2024 na aliaga akiwa na umri wa miaka 72.

Kulingana na familia, Lizzie alikuwa akiugua ugonjwa ambao hawakuutaja kwenye tangazo la kifo chake.

Kando na taasisi ya NIBS, Lizzie alikuwa akiendesha shule kwa jina “Lizzie Wanyoike Preparatory School” na ndiye mmiliki wa hoteli iitwayo “Emory”.

Mipango ya mazishi itatangazwa baadaye.

Website | + posts