Home Habari Kuu Mwanawe Jessica Mbalu azikwa

Mwanawe Jessica Mbalu azikwa

0

Mwili wa Benedict Mbalu mwanawe mbunge wa Kibwezi Mashariki Jessica Mbalu na Joseph Mutava ulizikwa jana Jumamosi Januari 20, 2024 nyumbani kwao huko Kibwezi.

Benedict Musyoka Mbalu aliaga dunia kwenye ajali mbaya ya barabarani Jumapili Januari 14, 2024 jijini Nairobi.

Akizungumza kwenye hafla ya mazishi, babake marehemu alielezea kwamba siku hiyo ya Jumapili, Benedict alimfahamisha kwamba alikuwa anakwenda kushiriki chakula cha mchana na marafiki asijue ilikuwa mara yao ya mwisho kuzungumza.

Joseph alifahamisha umati pia kwamba alikuwa anamzika mwanawe kwenye siku yake ya kuzaliwa Januari 20.

Jessica kwa upande wake alifungua hotuba yake kwa kumtakia mema mume wake kwenye siku yake ya kuzaliwa na akaelezea kwamba alikuwa anamwomboleza Benedict kama mama na wala sio kama mbunge wa eneo hilo.

Alisema imekuwa vigumu sana kwao kukubali kuondokewa na Benedict lakini akasema anampenda na atasalia kuwa kwenye moyo wake.

Mazishi ya Benedict yalihudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, Spika wa bunge la taifa Moses Wetangula, Gavana wa kaunti ya Makueni Mutula Kilonzo Junior na aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko kati ya wengine wengi.

Alhamisi Januari 18, 2024 ibada ya wafu kwa ajili ya Benedict iliandaliwa katika kanisa katoliki la St. John the Evangelist mtaani Karen kaunti ya Nairobi.

Website | + posts