Mwanaume mmoja wa Kenya Kevin Adam Kinyanjui Kangethe, amerejeshwa mjini ,Massachusetts nchini Marekani, ili kushtakiwa kwa mauaji ya mpenzi wake mwaka mmoja uliopita.
Kinyanjui ni mshukiwa mkuu kwa mauji ya mpenzi wake Margaret Mbitu ambaye mwili wake ulipatikana ndani ya gari lake, katika uwanja wa ndege wa Logan International Airport mjini Boston Oktoba 31 mwaka jana.
Kangethe alisafirishwa kwenda marekani siku ya Jumapili kwenda Boston kujibu mashtaka ya mauaji.
Kangethe, tayari amepokonywa uraia wa Marekani .
Mbitu alikuwa mtoaji wa afya ya huduama ya jamii mjini Massachusetts na alitoweka tarehe 30 Oktoba mwaka jana, kwenda kumtembelea Kangethe na baadaye akaripotiwa kutoweka .
Kulingana na uchunguzi wa awali Kang’ethe ni mshukiwa mkuu kwa mauji hayo, baada ya kupatikana na mali ya kibinafsi ya marehemu.