Home Habari Kuu Mwanasiasa wa upinzani Tanzania Ally Kibao auawa kikatili

Mwanasiasa wa upinzani Tanzania Ally Kibao auawa kikatili

0
kra

Mwili wa mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Ally Kibao aliyetekwa nyara kutoka kwa basi na wanaume waliojihami kwa bunduki, umepatikana viungani mwa jiji la Dar es Salaam.

Wakati ukipatikana, ulikuwa na majeraha ya kupigwa na kumwagiwa tindikali, kulingana na taarifa ya chama chake.

kra

Mauji ya Kibao, ambaye alikuwa mmoja wa maafisa wa chama cha upinzani Chadema, ulipatikana Jumamosi asubuhi, siku moja baada ya kutekwa nyara na wanaume wawili.

Kulingana na mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe, Kibao aliondolewa ndani ya basi akisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea mjini Tanga.

Kwenye taarifa kupitia mtandao wa X siku ya Jumapili, Rais Samia Suluhu Hassan alielezea kusikitishwa kwake kutokana na kifo hicho na kutaka uchunguzi wa kina na wa haraka ufanywe kubaini waliomuua Kibao.

Website | + posts