Home Habari Kuu Mwanasiasa wa ODM Narok Town afariki

Mwanasiasa wa ODM Narok Town afariki

0

Chama cha ODM Kinaomboleza kifo cha mwakilishi wadi wa Narok Town Lucas Kudake aliye pia mwanachama wa chama hicho ambaye amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.  

Katika taarifa kwa umma kupitia mtandao wa kijamii wa X Februari 16, 2024, ODM imesema Lucas Kudake ameaga dunia baada ya kupambana na maradhi kwa kipindi cha muda mrefu.

Chama hicho kimemuomboleza Kudake na kumtaja kama mwanachama aliyejitolea, mchapakazi, na mwaminifu ambaye alifanya kazi yake kwa nguvu na kuzidisha juhudi za kuimarisha chama cha ODM mashinani.

“Tunasikitika kutangaza kifo cha Mhe. Lucas Kudake, mwakilishi wadi wa Narok Town baada ya kuugua kwa muda mrefu. ODM imepoteza mwanachama aliyejitolea, mchapakazi na mwaminifu ambaye alifanya kazi kwa bidii na kukiweka chama imara mashinani. Tunaungana na familia yake kumuomboleza” Chama cha ODM kiliandika.

Kifo cha Kudake kina ujio wa wiki mbili tu baada ya mwenyekiti wa ODM Tawi la Githuri Joseph Kihara kuaga dunia. Kihara alizikwa Februari 7 nyumbani kwake Matuguta, Kaunti ya Kiambu.

Website | + posts