Home Habari Kuu Mwanasheria Mkuu aishauri KRA kusitisha matozo ya nyumba

Mwanasheria Mkuu aishauri KRA kusitisha matozo ya nyumba

0

Mwanasheria Mkuu Justin Muturi ameishauri mamlaka ya  ushuru nchini, KRA kusitisha ukusanyaji wa matozo ya nyumba baada ya mahakama ya rufaa kuharamisha ushuru huo Januari 26.

Kamishnaa Mkuu wa KRA Humphrey Wattanga, alikuwa amemwandikia Mwanasheria Mkuu mwezi Februari mwaka huu kutaka ushauri kuhusu uamuzi huo wa mahakama.

Akijibu barua hiyo, Muturi amesema kuwa KRA haipaswi kuendelea kukusanya ushuru wa nyumba kwani ni kinyume cha agizo la mahakama.

KRA ilikuwa imekusanya shilingi bilioni 26.8 katika kipindi cha miezi sita iliyopita ambazo ni wastani wa shilingi bilioni 4.47 kila mwezi.

Website | + posts