Home Kimataifa Mwanamume ahukumiwa miaka 20 jela kwa kumdhulumu mwanafunzi kimapenzi

Mwanamume ahukumiwa miaka 20 jela kwa kumdhulumu mwanafunzi kimapenzi

Kosa hilo linadaiwa kutekelezwa Septemba 8, 2021 katika eneo la Mwaoni, Diani kaunti ya Kwale.

0
Mwanamume ahukumiwa miaka 20 gerezani kwa dhuluma za kimapenzi.
kra

Mahakama moja ya Kwale imemhukumu Evans Oganda Ogega miaka 20 gerezani kwa kumdhulumu kimapenzi msichana mwenye umri wa miaka 15.

Kosa hilo linadaiwa kutekelezwa Septemba 8, 2021 katika eneo la Mwaoni, Diani katika kaunti ya Kwale.

kra

Hakimu Mkazi wa Kwale Ruth Ogolla alisema ushahidi uliowasilishwa na Allen Mulama, Wangari Mwaura, Nandi Rosemary na Collins Orwa ulikubalika na mahakama hiyo.

Mahakama hiyo ilifahamishwa kuwa Ogega alimvamia msichana huyo alipokuwa akiteka maji huku mama yake akiwa nje. Alimdhulumu kimapenzi na kufunika mdomo wa msichana huyo kwa nguo ili asiweze kuitisha usaidizi.

Kulingana na mahakama, mama ya msichana huyo alishangaa mbona mtoto wake amechelewa na alipoingia chumbani alimkuta mshukiwa akiondoka huku mwanawe akiwa amedhulumiwa.

Mama huyo aliwafahamisha majirani waliomvamia lakini maafisa wa polisi walimnusuru na kumpeleka katika kituo cha polisi cha Diani.

Hata hivyo, Ogega alikanusha mashtaka hayo akisema familia ya msichana huyo ilimsingizia.