Home Burudani Mwanamke mwingine ajitokeza kudai alitiwa mimba na Davido

Mwanamke mwingine ajitokeza kudai alitiwa mimba na Davido

0
kra

Mwanamuziki wa Nigeria Davido amehusishwa na mimba za wanawake wawili Anita Brown wa Amerika na Ivanna Bay kutoka Ufaransa na sasa mwingine amejitokeza.

Dada huyo kwa jina Chisom kwenye mtandao wa TikTok alisema aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Davido na akapata ujauzito. Alielezea kwamba Davido alimsihi aharibu mimba hiyo na kuahidi kumpa Naira milioni 3 ili asiseme jambo hilo.

kra

Chisom anasema hata baada ya kufanya alivyoambiwa, Davido hakumpa pesa alizoahidi. Alichapisha picha za mawasiliano yao kwenye WhatsApp pamoja na picha zao wakiwa pamoja kitandani.

Davido ambaye jina lake halisi ni David Adeleke Adedeji alitoa taarifa kupitia kwa msemaji wake kuhusu tuhuma za kwanza za kupachika kina dada wawili mimba akisema mawakili wake wanaendelea kudhibitisha uhalisia wake na kuchukua hatua. Davido alisisitiza umuhimu wa kushghulikia swala hilo kwa faragha na akaahidi kuwajibika ipasavyo.

Wafuasi wake wengi wanahisi kwamba yanayojiri yanaashiria kwamba anamkosea heshima mke wake Chioma ikitizamiwa kwamba ni miezi michache imepita tangu afiwe mwanawe wa kiume.

Website | + posts