Mwanaharakati Tony Gachoka jana Alhamisi aliwasilisha kesi ya tatu mahakamani kupinga kukodishwa kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA kwa mfanyabiashara wa India – Adani.
Gachoka pamoja na kundi lingine la majaji kutoka Mlima Kenya wanahoji kuwa mchakato huo haukufuata sheria na pia umma haukuruhusiwa kutoa maoni.
Gachoka ameishitaki kampuni ya Adani, Waziri wa Fedha John Mbadi, Mwanasheria Mkuu Dorcas Oduor, Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir na Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini.
Tayari, Mahakam Kuu imesitsha shughuli hiyo ya kukodishwa kwa uwanja wa JKIA na mstawishaji huyo wa kibinafsi, hadi pale kesi iliyowasilishwa itakaposikizwa na kuamuliwa.