Home Kaunti Mwanahabari wa Mediamax Catherine Wanjeri yuko katika hali nzuri

Mwanahabari wa Mediamax Catherine Wanjeri yuko katika hali nzuri

0
Mwanahabri wa Mediamax Catherine Wanjeri apigwa risasi akiwa kazini wakati wa maandamano kaunti ya Nakuru.
kra

Mwanahabari wa kampuni ya Mediamax Catherine Wanjeri Kariuki aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano dhidi ya serikali katika kaunti ya Nakuru, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji.

Kulingana na Mwenzake Mumbi Wambugu ambaye alizungumza na shirika la utangazaji nchini KBC kwa njia ya simu, Wanjeri awali alikuwa amepelekwa kwenye hospitali ya Valley lakini baadaye akahamishwa hadi hospitali kuu ya Nakuru.

kra

Wanjeri alipigwa risasi ya mpira mara tatu kwenye paja lake licha ya kuwa alikuwa amevalia sare rasmi ya wanahabari na kuvalia kitambulisho chake cha uanahabari. Kariuki anasemekana kuwa katika hali thabiti.

Kisa hicho kilishtumiwa vikali na wadau wa sekta ya vyombo vya habari ambaye walitaka hatua kuchukuliwa dhidi ya afisa wa polisi aliyehusika kwenye kisa hicho.

Rais wa chama cha wahariri wa habari Zubeida Kananu, na katibu mkuu wa chama cha wanahabari Eric Oduor , walitoa wito wa kulindwa kwa wanahabari wakiwa kazini.

Hata hivyo chama cha wanahabari nchini MCK, kiliwahimiza wanahabari kuzingatia usalama wao wanapokuwa kazini.

“Tunatoa wito kwa wanahabari kuhakikisha usalama wao na kutekeleza utaalam wanapofanya kazi katika mazingira hatari,” alisema afisa mkuu mtendaji wa MCk David Omwoyo.

Website | + posts