Mtangazaji wa kipindi cha mazungumzo ambaye alifungwa jela kwa kuhujumu uadilifu wa taifa la Burundi amesamehewa.
Floriane Irangabiye alikuwa ametumikia miezi 18 ya kifungo cha miaka 10 jela wakati ofisi ya rais ilipotangaza siku ya Alhamisi kwamba “inamuondolea kifungo hicho kamili”.
Kabla ya kukamatwa kwake, mwandishi huyo alikuwa akiishi katika nchi jirani ya Rwanda ambako aliendesha kampuni ya vyombo vya habari iitwayo Radio Igicaniro ambayo mara kwa mara iliikosoa serikali ya Burundi.
Wakati wa kukamatwa kwake miaka miwili iliyopita, alikuwa amerejea Burundi kuhudhuria mazishi ya mwanafamilia.