Home Habari Kuu Mwanahabari Rita Tinina kuzikwa Machi 27 Narok

Mwanahabari Rita Tinina kuzikwa Machi 27 Narok

0

Mazishi ya mwanahabari Rita Tinina aliyefariki mapema wiki hii yataandaliwa tarehe 27 mwezi huu katika kaunti ya Narok.

Ibada ya mazishi itafanyika nyumbani kwao Noosupeni Farm Olokirikira, kaunti ya Narok, kuanzia saa nne asubuhi na matayarisho ya mazishi yanaendelea kila siku kuanzia saa kumi na moja unusu jioni katika kanisa la All Saint’s Cathedral.

Misa ya wafu imeratibiwa kuandaliwa katika kanisa la Holy Family Basilica Machi 25.

Rita alikuwa binti ya marehemu Dominic na Mary Yiapan. Amemwacha binti Mia Malaikah.

Marehemu alipatikana amefariki chumbani mwake tarehe 17 mwezi huu.

Uchunguzi wa maiti yake umebaini kuwa mwanahabari huyo mahiri alifariki kutokana na nimonia kali.

Website | + posts