Kituo cha radio kinachopeperusha matangazo yake kwa lugha ya Kamba- Mbaitu, familia, mashabiki na marafiki wanaomboleza kifo cha mwanahabari Mercy Mawia aliyefariki jumanne tarehe 23 akipokea matibabu ya upasuaji katika hospitali ya Nairobi.
Kwa mujibu wa Mbaitu FM, ‘’ tunatangaza kwa huzuni kifo cha mtangazaji wetu wa kipindi cha Drive- Mercy Mawia, aka Kamuwetangi, aliyefariki usubuhi wa leo akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi baada ya kulazwa ili kufanyiwa upasuaji. Mumewe aliyekuwa kando yake wakati huo alithibitisha kifo hicho’’. Kituo hicho kilidhibitisha.
Mumewe James Mwangi aliyekuwa naye wakati akifariki, alisema kuwa mkewe alipigana vita vikali na hali yake ila alilemewa na kuaga dunia.
Wanahabari wenza kama vile aliyekuwa mtangazi wa KBC Bonnie Musambi, gavana wa Machakos Wavinya Ndeti wamemwomboleza kwa kumtaja kama kielelezo chema kwa wasichana na tasnia ya uwanahabari.