Home Kaunti Mwanafunzi afariki katika ajali Soy

Mwanafunzi afariki katika ajali Soy

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Otiende, eneo la Soy.

0

Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi ya St. Monica katika kaunti ndogo ya Likuyani kaunti ya  Kakameg, alifatiki baada ya kugongwa na  tinga tinga ya kubeba miwa Jumatano jioni.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Otiende, eneo la Soy.

Kulingana na chifu wa eneo hilo Boniventure Lugado, wanafunzi walikuwa wakielekea nyumbani kutoka shuleni ajali hiyo ilipotokea.

“Hatuwezi thibitisha chanzo cha ajali hiyo, lakini mwanafunzi alipatikana barabarani akiwa amefariki na dereva wa trekta hiyo akiwa ametoweka,” Lugado alisema.

Lugado aliwasihi madereva wa trekta wa kubeba miwa kuwa waangalifu wakiwa katika  barabara za vijijini, ili kuepuka ajali kama hiyo.