Home Habari Kuu Aliyekuwa mwakilishi wadi wa Huruma apatikana amefariki

Aliyekuwa mwakilishi wadi wa Huruma apatikana amefariki

0
Mwakilishi wadi wa zamani Lucy Chomba, apatikana amefariki. Picha/ Hisani.

Aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Huruma katika kaunti ya Uasin Gishu Lucy Nge’ndo Njoroge Chomba, amepatikana akiwa amefariki chumbani mwake eneo la West indies viungani mwa mji wa Eldoret.

Mwili wake ulitambuliwa na mmoja wa familia yake baada ya kukosa kuamka usubuhi na kuwajuza polisi.

Kamanda polisi wa kaunti ya Uasin Gishu Benjamin Mwanthi, alithibitisha tukio hilo na kusema kuwa maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi.

Kifo cha Lucy huenda kikaibua maswali mengi kwa kuwa mumewe Peter Chomba ambaye pia alikuwa mwakilishi wa wadi hiyo, alifariki miaka minne iliyopita kwa njia ya utata.

Inadaiwa alianguka chumbani mwake na kupoteza fahamu. Alipelekwa hospitalini lakini alifariki muda mfupi baadae.

Baada ya kifo cha Peter, naibu rais wa wakati huo ambaye sasa ni Rais wa taifa hili William Ruto,  alimpendekeza Lucy kuwania wadhifa huo katika uchaguzi mdogo kama heshima kwa familia ya mwenda zake.

Lucy alishinda na kumridhi muwewe hadi mwaka wa 2022.