Home Kimataifa Mwakilishi wa LSK katika JSC aapishwa

Mwakilishi wa LSK katika JSC aapishwa

0
kra

Wakili Samson Omwanza Ombati aliapishwa leo kama mwanachama wa tume ya huduma za mahakama JSC anayewakilisha chama cha mawakili nchini LSK.

Hafla fupi ya kumwapisha iliandaliwa katika mahakama ya upeo na kuongozwa na jaji mkuu Martha Koome. Omwanza anachukua mahala pa Macharia Njeru ambaye amekuwa akiwakilisha LSK katika JSC kwa miaka mitano iliyopita.

kra

Huku akimkaribisha kwa tume ya huduma za mahakama, jaji mkuu Koome alimtakia Ombati kila la kheri anapoanza kazi kama mwanachama wa LSK huku akimhimiza azingatie uadilifu na sheria ya haki.

Alimtaka akumbuke kiapo alichokula leo katika kuhakikisha wakenya wanapata haki siku zote.

Omwanza kwa upande wake alishukuru wote waliomuunga mkono alipowania wadhifa huo wa mwakilishi wa LSK katika JSC akiahidi kutumikia LSL, JSC na wakenya kwa uadilifu.

Alitambua wanachama wa LSK waliohudhuria uapisho wake akiwemo wakili wa serikali Shadrack Mose, mbunge Sylvanus Osoro na Isaac Ruto kati ya wengine ambao alisema wanasukumwa na shauku ya maslahi yao ndiposa wakafika.

Muhula wa Ombati katika JSC unaanza Mei 13, 2024 na atahudumu kwa muda wa miaka mitano kufuatia ushindi wake kwenye uchaguzi wa mwakilishi wa LSK uliofanyika Februari 29, 2024.