Home Kaunti Mvua kubwa yaharibu mapaa ya mabweni Migori

Mvua kubwa yaharibu mapaa ya mabweni Migori

0
Shughuli za masomo katika Chuo cha ualimu cha Migori zimesambaratika baada ya upepo kuharibu mapaa ya mabweni katika chuo hicho.
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule hiyo Dkt. Emily Kibbet, uharibifu huo umetatiza shughuli za masomo na kuwalazimisha kuwarundika pamoja wanafunzi bila kujali mwaka wao wa masomo.
Dkt. Kibbet alieleza kuwa hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa katika mkasa huo huku akisisitiza kuwa ilikuwa ni bahati nzuri kwamba ulitokea wakati wanafunzi hawakuwa karibu na bweni hilo wakati huo wa mvua nyingi.
Aliongeza kuwa uharibifu huo utagharimu shule hiyo zaidi ya shilingi milioni moja na kuomba idara husika kuingilia kati na kusaidia kurekebisha uharibifu huo kwa wakati ili wanafunzi chuoni hapo waweze kuendelea na masomo yao.
Celestine Mwango
+ posts