Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini imetahadhirisha kwamba mvua kubwa ya zaidi ya kina cha milimita 40 katika muda wa saa 24, ambayo kwa sasa inanyesha maeneo kadhaa nchini, huenda ikaendelea kunyesha kuanzia Alhamisi hadi Jumapili.
Katika ushauri wake, idara hiyo inasema mvua kubwa inatabiriwa kuenea katika maeneo ya kaskazini mwa nchi.
Maeneo ambayo yametabiriwa kushuhudia mvua kubwa ni pamoja na kaunti za Nandi, kericho, Kakamega, Nairobi, Nyeri, machakos, kitui Kajiado, Marsabit, Nyandarua, marsabit, Laikipia na Vihiga miongoni mwa kaunti zingine.
Mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Dkt David Gikungu, alisema upepo mkali wa kusi wenye zaidi ya kasi ya mita 20 kwa kila sekunde, unatarajiwa katika eneo la Pwani na maeneo ya Kaskazini-Mashariki mwa Kenya.
Anasema kuwa upepo mkali unatarajiwa kuzidi kasi ya mita 20 kwa kila sekunde siku ya Alhamisi hadi Jumapili na mawimbi makubwa ya bahari ya zaidi ya mita mbili yaliyotabiriwa katika bahari ya Hindi kuanzia Alhamisi hadi Jumapili.
Dkt. Gikungu anawataka wananchi kuwa macho dhidi ya mafuriko yanayoweza kutokea na hata ukungu, akiongeza kuwa viwango vya maji katika mito, maziwa na mabwawa vinatarajiwa kuongezeka.
Dkt. Gikungu anaomba umma kujiepusha kuendesha magari katika maeneo yanayofurika, au kutembea katika maji yanayosonga.
Na inapaswa kuepuka kutembea katika maeneo wazi au kujikinga chini ya miti na karibu na madirisha ya chuma yaliyochomwa ili kupunguza uwezekano wa kupigwa na radi.
Amewataka wananchi kuwa waangalifu katika maeneo yanayokabiliwa na maporomoko ya ardhi na matope kwani udongo bado ni umelowa maji na inaweza kuwa hatari.