Home Habari Kuu Umoja wa Ulaya wasitisha ushirikiano wa kiusalama na Niger

Umoja wa Ulaya wasitisha ushirikiano wa kiusalama na Niger

0
kra

Umoja wa Ulaya, EU umetangaza kwamba umesimamisha ushirikiano wote wa kiusalama na taifa la Niger baada ya jeshi la nchi hiyo kutwaa mamlaka kupitia mapinduzi.

Haya yanajiri muda mfupi baada ya Marekani kutangaza kwamba inamuunga mkono Rais aliyebanduliwa mamlakani Mohamed Bazoum anayechukuliwa kuwa rafiki wa mataifa ya magharibi katika vita dhidi ya makundi ya kigaidi ya kiisilamu.

kra

Ijumaa wiki iliyopita, mkuu wa kitengo cha ulinzi wa Rais nchini Niger Jenerali Abdourahmane Tchiani alijitangaza kuwa kiongozi wa nchi hiyo huku akisema alichochewa na ukosefu wa usalama, kuzorota kwa uchumi na ufisadi kutwaa mamlaka.

Kwa sasa, kuna wasiwasi kati ya mataifa ya magharibi kuhusu nchi atakazochagua kushirikiana nazo kiongozi huyo.

Nchi jirani za Burkina Faso na Mali zimekuwa zikishirikiana na Urusi tangu mapinduzi.

Mkuu wa kitengo cha sera za kigeni katika EU Josep Borrell amejiunga na Marekani na Ufaransa katika kukataa kutambua viongozi wa mapinduzi, na kuongeza kwamba ushirikiano wa kiusalama na kifedha umesimamishwa kwa muda usiojulikana.

Ufaransa ambayo Niger ilikuwa koloni yake ilitangaza kusitishwa kwa misaada yote ya kimaendeleo na kifedha huku Umoja wa Afrika ukiwataka wanajeshi wa Niger warejee kambini katika muda wa siku 15.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken Ijumaa juma lililopita alionya wanaomzuilia Rais Bazoum, kiongozi wa kwanza aliyechaguliwa aliyechukua mahala pa kiogozi mwingine aliyechaguliwa nchini humo.

Website | + posts