Home Habari Kuu Muungano wa Azimio wazindua tovuti ya kukusanya sahihi

Muungano wa Azimio wazindua tovuti ya kukusanya sahihi

0

Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, umezindua tovuti ya kuendeleza na kuboresha mpango wa kukusanya sahihi milioni 15. Uzinduzi wa tovuti hiyo www.tumechoka.com ulifanyika leo katika afisi za kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka maarufu kama SKM Command Centre mtaani Karen.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, kiongozi wa Azimio Raila Odinga alisema kwamba jukwaa hilo la kidijitali litapiga jeki majukwaa na mipango mingine kama vile maandamano na kukwepa kulipa ushuru inayolenga kulazimisha serikali kurekebisha au kutupilia mbali sheria ya fedha ya mwaka 2023 na kuchukua hatua za kupunguza gharama ya maisha.

Mhe. Odinga akitia sahihi kwenye tovuti waliyozindua

Viongozi wengine ambao walihudhuria uzinduzi wa tovuti hiyo ni pamoja na kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua, kiongozi wa chama cha DAP- K Eugene Wamalwa na gavana wa zamani wa kaunti ya Murang’a Mwangi Wa Iria.

Aliyekuwa Gavana wa Kakamega Wyckliffe Oparanya, aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni, aliyekuwa gavana wa Laikipia Nderitu Muriithi na kiongozi wa wachache bungeni Opiyo Wandayi pia walikuwepo.

Mpango wa kukusanya sahihi ulianzishwa kwenye mkutano wa saba saba Ijumaa iliyopita ambapo kiongozi wa Azimio Raila Odinga alisema lengo lilikuwa sahihi milioni 10 lakini akihutubia wanachi jijini Nairobi jana, kiongozi huyo alisema sasa wanalenga sahihi milioni 15.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here