Home Habari Kuu Muungano wa Azimio wasema utashiriki katika maandamano ya Madaktari

Muungano wa Azimio wasema utashiriki katika maandamano ya Madaktari

Muungano huo unamtaka waziri wa afya Susan Nakhumicha kujiuzulu kutokana na kile ulikitaja kuwa utepetevu kazini na kushughulikia visivyo mgomo unaoendelea wa madaktari.

0
Viongozi wa Azimio watishia kushiriki katika maandamano ya Madaktari.

Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, leo Jumanne umesema kuwa zaidi ya wagonjwa 500 wameaga dunia kutokana na mgomo wa kitaifa wa madaktari unaoendelea.

Kutokana na hayo, muuongano huo umesema utaungana na madaktari katika maandmano yao, iwapo serikali haitatatua malalamishi yao.

Ukiongozwa na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, muungano huo unamtaka waziri wa afya Susan Nakhumicha kujiuzulu kutokana na kile ulikitaja kuwa utepetevu kazini na kushindwa kushughulikia mgomo unaoendelea wa madaktari.

Wakizungumza na wanahabri jijini Nairobi, viongozi wa muungano huo walisema serikali imepuuzilia matakwa ya madaktari, huku wakitoa wito wa kuimarishwa kwa  maslahi ya madaktari hao.

“Serikali inapaswa kuwekeza katika vifaa vinavyohitajika vya matibabu pamoja na kuimarisha usambazaji wa vifaa vya matibabu ili kuboresha utoaji huduma za afya hapa nchini,” walisema viongozi hao.

Kulingana na muungano huo, mgomo wa madaktari umetatiza utoaji huduma za afya na kwamba wananchi wengi wanateseka kutokana na hali hiyo.

Website | + posts