Home Habari Kuu Umoja wa Afrika washutumu jaribio la mapinduzi Niger

Umoja wa Afrika washutumu jaribio la mapinduzi Niger

Hali hiyo ilisababisha makabiliano makali kati ya wanajeshi wanaomuunga mkono Rais na wale wanaompiga na kuchangia kujerujiqa kwa mtu mmoja.

0
kra

Umoja wa Afrika, AU umeshutumu jaribio la mapinduzi ya serikali nchini Niger.

Baadhi ya walinzi wa Rais Mohamed Bazoum walimgeuka, kumfungia na kumzuia kuondoka katika kasri lake mjini Niamey.

kra

Hata wafanyakazi wa ikulu walizuiliwa kutoka nje.

Hali hiyo ilisababisha makabiliano makali kati ya wanajeshi wanaomuunga mkono Rais na wale wanaompinga na kuchangia kujeruhiwa kwa mtu mmoja.

Mwenyekiti wa AU Musa Faki ameshutumu jaribio hilo akisema ni usaliti mkubwa kwa raia wa Niger na kutaka wahusika kusitisha vitendo hivyo.

Website | + posts