Home Kimataifa Muthoni: vifaa zaidi vya matibabu vimepelekwa kaunti ya Nyeri

Muthoni: vifaa zaidi vya matibabu vimepelekwa kaunti ya Nyeri

Muthoni alithibitisha kuwa wizara hiyo imefungua kituo cha kutoa huduma za dharura, na kupeleka makundi maalum ya kushughulikia masuala ya dharura.

0
Katibu wa afya ya umma Mary Muthoni.
kra

Wizara ya afya imesema itatoa vifaa vya matibabu vinavyohitajika, katika hatua ya kushughulikia waathiriwa wa mkasa wa moto uliotokea katika shule ya Hillside Endarasha kaunti ya Nyeri.

Katibu katika wizara ya afya ya umma Mary Muthoni, alisema wizara hiyo itatoa huduma za kisaikolojia na ushauri nasaha kwa waathiriwa, familia zao, manusura na wanaotoa huduma ya kwanza.

kra

Muthoni alithibitisha kuwa wizara hiyo imefungua kituo cha kutoa huduma za dharura, na kupeleka makundi maalum ya kushughulikia masuala ya dharura.

Akizungumza katika kanisa la St Pauls  ACK la Kirinyaga wakati wa mkutano kati ya viongozi wa kanisa na wahudumu wa afya ya umma, Muthoni alisema wizara hiyo imewapekela wahudumu wa afya  kusaidia serikali ya kaunti ya Nyeri kushughulikia mkasa wa moto uliotokea jana katika shule ya HillSide Endarasha.

Alidokeza kuwa kundi la ushughulikia dharura tayari linasaidia kuwatafuta wanafunzi ambao hawajulikani waliko, na pia kusaidia familia zao.

Aliwahimiza wananchi kupiga simu kutumia namba maalum 719 bila malipo, kuomba msaada au kutoa habari zozote zinazohusiana na mkasa huo.

Website | + posts