Home Habari Kuu Museveni avisifu vyombo vya usalama kwa kuzima maandamano

Museveni avisifu vyombo vya usalama kwa kuzima maandamano

0
kra

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewasifu maafisa wa vyombo vya usalama nchini humo kwa kuzima na kuwakamata waliohusika na maandamano ya kulalamikia ufisadi nchini humo.

Katika taarifa iliyochapishwa katika ukarasa wake wa X zamani Twitter, Museveni amedai kuwa maandamano hayo yamepangwa na “mashirika ya kigeni yanayolenga kuendeleza ukoloni mamboleo”.

kra

“Jambo la pili, ni kwamba baadhi ya waandalizi na washiriki wa maandamano hayo, walikuwa wakipanga mambo mabaya sana dhidi ya watu wa Uganda. Mambo mabaya sana hayo, yatadhihirika mahakamani wakati waliokamatwa watakapofunguliwa kesi. Inawezekana, kwamba baadhi ya washiriki, hawakujua kuhusu fedha kutoka nje zilizofadhili maamdamano hayo na mambo mabaya yaliyopangwa. Ndio maana, walipaswa kusikiliza ushauri wa polisi, sio kuendelea na maandamano. Lakini walipuuza ushauri wa polisi,” sehemu ya taarifa hiyo imesema.

Rais huyo pia ameongeza kusema “Vinginevyo, yangekuwa maandamano ya kizalendo, ya kupinga ufisadi, ya amani, yaliyoratibiwa na Polisi, ningekuwa wa kwanza kujiunga nayo”.