Home Burudani Museveni aingilia kati kuokoa tamasha ya Nyege Nyege

Museveni aingilia kati kuokoa tamasha ya Nyege Nyege

0

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameingilia kati kuokoa tamasha maarufu ya Nyege Nyege baada ya mabalozi wa kigeni kuwaonya raia wao dhidi ya kuhudhuria tamasha ya mwaka huu kwa hofu ya mashambulizi ya kigaidi.

Tamasha hiyo iliratibiwa kuanza mjini Jinja, kilomita 80 kutoka Kampala Alhamisi iliyopita.

Museveni amewahakikishia raia wake na wote watakaohudhuria tamasha hiyo kwamba itakuwa salama na hakuna haja ya kuhofia na kukosa kuhudhuria.

Ameongeza kuwa tayari maafisa wa usalama wa kutosha watashika doria wakati wa tamasha hiyo.

Website | + posts