Home Michezo Museveni afungua uga wa Nakivubo tayari kwa AFCON 2027

Museveni afungua uga wa Nakivubo tayari kwa AFCON 2027

0

Uwanja wa Nakivubo umefunguliwa rasmi siku ya Ijumaa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, tayari kwa maandalizi ya kipute cha AFCON mwaka 2027 na CHAN baadaye mwaka huu.

Museveni amefungua uga huo wa Nakivubo War Memorial unaoselehi mashabiki 35,000.

Rais Museveni amemsifia mkandarasi aliyefanya ukarabati wa uwanja huo Hamis Kiggundu, kwa kukamilishakazi kwa wakati ufaao.

Uwanja wa Nakivubo

Museveni alifuchua pia kuwa serikali yake inalenga kufungua upya uwanja wa Nelson Mandela- Namboole, ambao unafanyiwa ukarabati ulio kamilika kwa asilimia 95.

Museveni aliahidi kujenga angaa viwanja vingine viwili, kabla ya kuandaa fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2027.

Uganda itaandaa AFCON ya mwaka 2027 kwa pamoja na majirani Tanzania na Kenya kwa mara ya kwanza.