Home Habari Kuu Murkomen: Serikali inajizatiti kukabiliana na ajali za barabarani

Murkomen: Serikali inajizatiti kukabiliana na ajali za barabarani

0
Waziri wa Uchukuzi na Barabara Kipchumba Murkomen.

Waziri wa uchukuzi na barabara Kipchumba Murkomen, ametoa wito kwa wakenya kuwa watulivu huku serikali ikijizatiti kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani.

Murkomen, ambaye alielezea wasiwasi wake kuhusu jinsi wanafunzi wanasafirishwa, alisema kuwa serikali itatoa mwongozo wa jinsi uchukuzi wa wanafunzi unapaswa kutekelezwa ikizingatiwa ajali za hivi majuzi zilizohusisha wanafunzi wa shule ya upili ya Chavakali, Kapsabet na Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Akizungumza katika shule ya upili ya  wasichana ya Mugoiri katika kaunti ya Muranga, waziri huyo alisema shule zinapaswa kuwajibikia usalama wa magari na usimamizi wa madereva wao.

“Tutatumia teknolojia kufuatilia usimamizi wa magari ya shule, huku magari hayo yakiwekwa kifaa cha ‘telematics’,” alisema waziri huyo.

Alisikitishwa na idadi inayoongezeka ya maafa kutokana na ajali za barabarani kila mwaka.

Website | + posts