Home Biashara Multichoice yataka serikali kumaliza wizi wa hakimiliki

Multichoice yataka serikali kumaliza wizi wa hakimiliki

0

Kuna haja ya serikali kuingilia kati na kumaliza wizi wa hakimiliki za sekta ya sanaa ili kuinusuru dhidi ya kuporomoka.

Haya ni kwa mjibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Multichoice Kenya Nzola Miranda .

Nzola amefuchua kuwa kampuni zinazotegemea kununua na kupeperusha vipindi vya runinga hupata hasara kubwa, kutokana na gharama kubwa wanayowekeza kununua lakini vipindi hivyo hutumiwa na walaghai ambao hawanunui vipindi hivyo bali huvitumia kupata hela.

Nzola amekariri kuwa wako tayari kushirikiana na serikali kwa hali mali, ili kumaliza wizi huo wa haki miliki ambayo inatoa ajira kwa mamilioni ya vijana nchini.

Kulingana na takwimu kutoka ka shirika Patners against Piracy PAP, serikali pamoja na sekta ya filamu na burudani hupata hasara ya shilingi bilioni 92 kw akila mwaka sawia na shilingi milioni 252 kwa kila siku kuptia kwa video,filamu na muziki zinazoigwa au kuibwa.

Ni kwa sababu hii ambapo wadau wa sekta hii wameandaa mswaada wa pamoja ambao unapendekeza mabadiliko ya sheria za wizi wa mitandaoni wa hakimiliki.

Baadhi ya mapendekezo ni kufunga mitandao yote ya Internet inayotekeleza wizi huo.

Website | + posts