Aliyekuwa muigizaji wa filamu maarufu nchini Nigeria John Okafor, maarufu kama Mr. Ibu, hatimaye alizikwa jana zaidi ya miezi mitatu tangu afariki Machi 2 mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Okafor alizikwa nyumbani kwake Amuri katika jimbo la Enugu huku mazishi hayo yakihudhuriwa na rafiki, jamii na mashabiki wake.
Waigizaji wengine maarufu kama vile Patience Ozokwor na Angela Okorie pia walihudhuria mazishi hayo.
Mr. Ibu amekuwa akiugua tangu mwezi Oktoba mwaka 2023 na alifanyiwa upasuaji mara kadhaa na baadaye kukatwa miguu yote.