Waziri mwenye Mamlaka Makuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi, anatarajiwa kuondoka nchini Jumapili jioni kuelekea mjini Windhoek, Namibia kwa ziara rasmi ya kiserikali.
Mudavadi atakutana na Makamu Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ndaitwah, kujadilaina kwa kina kuhusu kuimarisha kwa ushirikiano baina ya Kenya na Namibia.
Wakati wa mkutano kati yao, makubaliano na mwafaka wa kibiashara uliopo kwa sasa kati ya nchi hizo mbili pia utapitiwa upya.
Akiwa ziarani nchini Namibia, Mudavadi pia anatarajia kumpigia debe Raila Odinga anayewania uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AUC.